Mbunge ataka bunge liahirishwe kwa tetemeko la Kagera, Naibu Spika agoma

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ametaka Bunge kuharishwa kufuatia hali mbaya ya wakazi wa Mkoa wa Kagera kufiatia kutokea kwa tetemeko là ardhi lilosababisha madhara makubwa.

Heche alileta hoja hiyo baada ya kuomba muongozo wa Spika kupitia kifungu namba 47 kwakile alichodai kuwa serikali kushindwa kutoa tamko lolote licha ya kutembelea eneo là tukio

Hâta hivyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson amekataa hoja hiyo kwakile alichosema kuwa kwakuwa katika orodha ya shughuli za Bunge leo kuna kauli ya mawaziri hivyo wasubiri kwanza kauli hiyo endapo hawatakubaliana nayo ndiyo walete hoja.