Mkazi wa buguruni kwa mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Ilala na kusomewa tena shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha .
Scorpion ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Ally mkazi wa mabibo Hostel, alipandishwa kizimbania mahakamani hapo kwa mara ya kwanza September 23 mwaka huu.
Kesi hiyo inayosikilizwa na hakimu Adolf Sachore leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Source: Mwananchi