Mariah Carey anaweza kubaki na pete ya dola milioni 10 aliyovishwa na mchumba wake James
Packer waliyeachana. Lakini hiyo haitoshi, muimbaji anataka zaidi.
Wawili hao waliachana baada ya kuzuka ugomvi walipokuwa wakila bata kwenye yacht nchini
Ugiriki mwezi September kufuatia tetesi kuwa diva huyo anachepuka na dancer wake, Bryan
Tanaka.
Kwa mujibu wa ripoti, Carey anataka alipwe dola milioni 50 kutoka kwa Packer baada ya
kumhamishia LA na anadai kuwa ameathirika na
kuachana kwao kiasi cha kukatisha ziara yake ya Amerika Kusini.
Hata hivyo vyanzo vilivyo karibu na bilionea huyo vimedai kuwa Carey asahau kupewa hata senti.
“Ni ujinga kudai kuwa James ni sababu ya kusitisha ziara yake ya Amerika Kusini. Siku
chache zilizopita aliwalaumu mapromota,”
kilisema chanzo.
Sababu kubwa inayoelezwa kuwa chanzo cha wawili hao kuachana ni usaliti wa Carey na
matumizi makubwa ya fedha. Wawakilishi wa
muimbaji huyo wanakanusha