MAJALIWA AMSHUKIA RC MAKONDA KWA KUMTUHUMU KAMANDA SIRRO KUWA AMEHONGWA NA WAUZA SHISHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemataka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusimamia maagizo anayopewa na wakuu wake na kuacha kulalamika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana wakati akizindua Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam naye alikuwepo.

Alipokua akiongea katika uzinduzi wa mradi huo, Paul Makonda alimtuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kuwa hawatekelezi maagizo yake anayopa kuhusu kupambana na wauza dawa za kulevya aina ya shisha.

Paul Makonda alisema kuwa wafanyabishara 10 walimfuata wakitaka kumuhonga shilingi milioni 5 kila mmoja kwa mwezi lakini alikataa, hivyo kitendo cha Makamishna hao wa Polisi kusua sua kutekekeleza maagizo yake, huenda wao wamekubali kupokea fedha hizo (kuhongwa).

Akisimama kujibu salamu hizo za mkuu wa mkoa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Makonda kutekeleza maagazo anayopewa kwani yeye ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa hivyo akipewa maagizo ahakikishe anafikisha kwa walioko chini yake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Paul Makonda kuhakikisha kuwa anailinda miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) jijini Dar es Salaam.