Eric Aniva alikiri kufanya mapenzi na wanawake pamoja na wasichana 104
Uamuzi wa kesi ya mwanamme mmoja nchini Malawi unatarajiwa kutolewa wiki hii, baada ya kuiambia BBC kuwa alifanya mapenzi na wasichana kama sehemu ya mila.
Eric Aniva alikamatwa mwezi Julai kufuatia amri ya rais, baada ya kukiri kuwa alifanya mapenzi yasiyo na kinga na wasichana walio na umri wa hadi miaka 12, na kuwa kimya juu ya hali yake ya kuugua ugonjwa wa ukimwi.
Aniva anasema kuwa alipewa vibarua na familia za wasichana hao kushiriki mapenzi nao, kwa tamaduni ambayo jamii inaamini kuwa huwezesha wasicha kuingia utu uzima.
"Tunaamini kuwa ikiwa mjane au mwanamme aliyefiwa hawezi kusafishwa kwa njia ya mapenzi, huenda kisa kibaya kikafuatia kama kifo kwa majane au mwanamme aliyefiwa au kwa ukoo mzima," alisema mhudumu mmja wa jamii.Image captionMalawi
Wakati rais wa Malawi Peter Mutharia aliamrisha mwanamme huyo akamatwe, alitaka Aniva ashtakiwe kwa kuwabaka wasichana wadodgo, lakini hata hivyo hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.
Kwa hivyo sasa Aniva ameshtakiwa kwa kushiriki utamaduni wenye kuumiza, chini ya kipengee cha chato cha sheria ya usawa wa kijinsia nchini Malawi ambapo alifanya mapenzi na wajane.
Katika kesi hii wanawake wawili wamejitokeza ili kutoa ushahidi dhdi ya Aniva, licha ya mmoja kusema kuwa alifanya mapenzi naye kabla ya mila hiyo kupigwa marufuku huku mwingine naye akisema kuwa alifanikiwa kukimbia kabla ya kitendo cha ngono kufanyika.
Hadi miaka michache iliyopita, mila hii ilikuwa maarufu katika wilaya yote kwa mjane kufanya mapenzi na mwanamme mara tatu kwa siku kwa usiku tatu au nne.Image copyrightAFPImage captionEric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti
Mwanamme huyo anaweza kuwa ndugu wa mmewe, lakini wakati mwingine mtu kutoka nje hutafutwa kama Aniva kuweza kushiriki kitendo hicho.
Ikiwa aliyefiwa ni mwanamme, mwanamke hutafutwa kuweza kufanya mapenzi naye.
Kinachowatisha watu nchini Malawi kuhusu Aniva, ambaye alidai kufanya mapenzi na wanawake 104 pamoja na wasicha, wakati wa mahojiano na BBC ni kuwa hukuachana na tabia hiyo licha ya kugundua kuwa alikuwa na virusi vya HIV
"HIV inaua. Itakuwaje mtu mwenye virusi kufanya kile alichokifanya? Nafikiri yeye ni shetani. Ningekuwa hakimu ningempa hukumu ya kifo na kifungo cha maisha," alisema mhubiri Paul Mzimu.