PICHA: DONALD TRUMP AKIWA NA BONDIA MSTAAFU, FLOYD MAYWEATHER

Viongozi wengi sana kwa sasa wanagombania nafasi ya kukutana na aliyechaguliwa kuwa Rais nchini Marekani na kuchukua nafasi ya Rais Barack Obama aliyeko Ikulu kwa sasa, Bwana Donald Trump, lakini cha kushangaza mfanyabiashara huyo bilionea nchini humo,  amepata nafasi hiyo ya kukutana na Floyd Mayweather ambaye ni Bondia mstaafu na.
Bondia huyo mstaafu alikuwa nchini New York ku’promote’ shindano la ngumi kati ya Badou Jack na Brit James DeGale .
Trump na Mayweather waliweza kupata wasaa wa kupiga picha wakiwa na mtoto wa Trump, Donald Trump Jr katika moja ya ofisi zilizoko katika jengo la Trump (Trump Towers).
Aidha, Trump alikuwepo pia katika mpambano uliofanyika mwaka jana kati ya Floyd Mayweather na mpinzania wake Manny Pacquiao.
Tangu amshinde Hillary Clinton katika uchanguzi uliomaliza Novemba 8 mwaka huu, Donald Trump kwa sasa yuko katika hatua za kukusanya timu atakayofanya nayo kazi katika Ikulu ya Marekani anayotarajiwa kuanza kazi ifikapo Januari 20, 2017.
Donald Trump akiwa na mkewe Melania Trump wakati wa mpambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao
Donald Trump akiwa na mkewe Melania Trump wakati wa mpambano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao