Polisi Dar Yaeleza kwa Nini Hawajamkamata Tundu Lissu

DAR ES SALAAM: Jana, Novemba 4, 2016 iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama baada ya kutotimiza masharti ya Mahakama kwa kutohudhuria kwenye kesi yake inayomkabili Kisutu, Dar.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamishna wake Simon Sirro imesema sababu za kwanini Tundu Lissu hajakamatwa mpaka sasa ni kutokana na Polisi kutopokea hati yoyote kutoka Mahakamani Kisutu inayoagiza kukamatwa kwa Tundu Lissu lakini ikiwafikia tu watafanya hivyo.