Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma hali iliyozua taharuki miongoni mwa watumishi wa kada mbalimbali nchini.
Inadaiwa kuwa baadhi ya watumishi wamekuwa wakidanganya taarifa zao za ndoa ili kujipatia nauli na stahiki nyingine za likizo.
Mwalimu mmoja katika Manispaa ya Ilala amesema uhakiki huo umepanga kuchelewesha zaidi malipo na stahiki za likizo za Waalimu ambazo hazijalipwa.
Akihojiwa na gazeti la Mtanzania Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Gratian Mukoba alisema bado hajapata taarifa kuhusu uhakiki huo wa vyeti vya ndoa isipokuwa kama utafanyika litakuwa ni jambo jema.