Watu watatu wamefariki dunia na zaidi ya 20 wamejaruhiwa kufuatia ajali ya basi la National Express iliyotokea eneo la Tumuli mkoani Singida leo asubuhi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa ajali ya basi hilo ambalo hufanya safari zake kati ya Iramba na Dar es Salaam, na leo lilikuwa likitokea Iramba mkoani Singida kuja Dar es Salaam. Miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na dereva wa basi hilo.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.