Msanii wa filamu nchini Jackline Wolper amekutana na kamera ya eNewz lakini katikati ya mahojiano alipokea simu ya mpenzi wake Harmonize kitendo ambacho kiliwaziba watu wengi midomo kutokana na wawili hao kudhaniwa kuwa hawakuwa wapenzi kweli.
Pia amemzungumzia mpenzi wake huyo na kusema kuwa ana wivu sana ndiyo maana hajaona shida kupokea simu yake katikati ya interview ili asimfikirie vibaya.
“Baby i’m good niko kwenye interview niko katikati ya shot nipe 5 minutes I will call you back”
Jackline Wolper pia amezungumzia kazi yake ya movie na kusema kwamba kwa sasa inabidi wajipange upya na waangalie sehemu waliyokosea huku akisisitiza kuwa bongo movie haijafa.
“Bongo movie haijafa na ninachoona inabidi tuangalie tulipoanguka pale tulipokosea then tujirekebishe lakini movie bado zipo na hazijafa”
Jackline Wolper ni kati ya wasanii wa bongo movie ambaye wenye uwezo mkubwa wa kuigiza.