Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti UHURU IRINGA Bw. Frank Kibiki amefariki

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti UHURU IRINGA Bw. Frank Kibiki amefariki jioni ya jana jijini Dar Es Salaam


ALIYEKUWA mwaandishi wa habari wa gazeti linalomilikiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM), UHURU, Bw. Frank Kibiki amefariki jioni ya jana jijini Dar Es Salaam mara baada ya kuugua ghafla. Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu alikuwa akiugua ugonjwa wa malaria kwa zaidi ya siku tatu na alikuwa akipata matibabu jijini Dar Es Salaam.


Marehemu Kibiki pia alishiriki ktk kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya kuwakilisha jimbo la Iringa mjini ktk nafasi ya ubunge. Taarifa zaidi endelea kuperuzi tovuti hii  au fatilia taarifa zetu za habari.