Mjumbe baraza kuu la Taifa CUF asema hawapo tayari kuona chama kinagawanyika.

Mjumbe wa  baraza kuu la Taifa la Chama Cha Wananchi CUF Mh Shaban Kaswaka   amesema licha ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu ndani ya chama hicho, hawatakuwa tayari kuona  baadhi ya viongozi wa juu wa CUF wakikigawanya chama hicho kwa maslahi yao binafsi bila kujali maslahi mapana  kwa wanachama wake.

Mjumbe huyo wa baraza kuu la CUF ambaye si miongoni mwa waliosimamishwa na chama hicho amesema hayo akiwa amefuatana  na makatibu wa wilaya wa chama hicho ambapo amesema katibu mkuu wa chama hicho  analengo la kukigawa chama hicho ambacho kwa sasa kinapitia wakati mgumu wa kisiasa.