Wafugaji watishia kunywa sumu wakipinga Ng’ombe wao kupigwa chapa

Wakati zoezi la kupiga chapa Ngo’mbe likiendelea kutekelezwa katika sehemu mbalimbali mkoani Morogoro wafugaji wanaounda kata tisa za tarafa ya Magole wilayani Kilosa wametishia kunywa sumu endapo zoezi hilo halitasitishwa huku wakidai kutoshirikishwa katika utekelezwaji wa zoezi hilo.

Wakuzungumza huku wakiangua vilio wafugaji hao wakiwemo wanawake wamesema katu hawakubaliani na  zoezi hilo kwani limekuwa likiwatia hasara  kila linapokuwa linatekelezwa.

Malahi Charahani ni mwenyekiti wa wafugaji wa tarafa hiyo ambaye ameiomba serikali kuona namna ya kusimamisha zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji juu ya zoezi hilo.