TETEMEKO LA ARDHI LATOKEA KANDA YA ZIWA -LASABABISHA MADHARA BUKOBA,ANGALIA PICHA

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera zinasema kuwa kuna tetememko la ardhi limetokea na kusababisha madhara makubwa.



Taarifa za awali zinasema kuna vifo vya watu vimetokea ingawa hatujaambiwa idadi kamili.


Inaelezwa kuwa nyumba kadhaa zimebomoka na majeruhi wengi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Tetemeko hilo la ardhi linadaiwa kupita katika mikoa mingine ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza na Shinyanga.

Taarifa kamili tutawaletea hivi punde...Tazama picha nyumba zikiwa zimebomoka huko Bukoba