WAZIRI
wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amemtaka mkuu wa magereza
mkoa wa Kagera(RPO) kamishna mwandamizi Jeremiah Nkonda kuwahamisha
wafungwa walioko katika gereza la Kitengule la wilayani Karagwe na
lililo tokea hivi karibuni mkoani hapa na kuharibu miundombinu na
mabweni ya kulala wafungwa katika gereza hilo.
Waziri Nchemba
alisema kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya siku moja Mkoani hapa
na kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake Kwa lengo la kuona
uharibifu uliojitokeza kutokana na tetemeko hilo .
"Nimetembelea
magereza yetu lakini gereza la Kitengule limeharibika sana, kuta
zimeanguka mabweni yameharibika Kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba
hawapaswi kuishi watu kwa hiyo,naagiza mkuu wa magereza hapa kuwahamishia
wafungwa hawa katika gereza la Mwisa lenye mabweni manne yaliyoko
wazi"Alisema Nchemba.
Alisema ndani ya wiki moja zoezi hilo liwe
limekamilika kwani wakiendelea kuwaaacha wafungwa hao humo ni hatari
kwani wanaweza kudondokewa na kuta zinazoning'inia na kusababisha
kuwapoteza watu hao.
Alisema kutokana na tukio hilo Wizara
inaandaa mpango wa Muda mrefu wa kujenga bweni kubwa litakalokuwa na
uwezo wa kubeba wafungwa 400 Kwa wakati mmoja kwani hilo ni gereza la
kikazi ambalo linabeba watu wengi.
Mkuu wa magereza mkoa wa
Kagera kamishna mwandamizi Jeremiah Nkonda alisema kilichochangia Sana
kushuka Kwa kuta hizo ni kwamba matofali yaliyojenga kuta hizo
yanaonekana yalijengwa Kwa tofali mbichi kwahiyo Kwa halii hiyo
haitowezekana kufanya ukarabati bali nikuhakikisha Wamebomoa mabweni
hayo na kujenga upya.
Alisema gereza hilo lilikuwa na uwezo wa
kubeba wafungwa 380 Kati ya hao 100 wako Kwenye kambi ndogo ambapo 280
ndo watakaohamishiwa katika gereza la Mwisa.