Baada ya Amini kudai msanii mwenzake Linah Sanga amebadilika na kupoteza ule uimbaji wake wakuvutia, Linah amefunguka na kuizungumzia kauli hiyo.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Ole Themba’ amesema kwa sasa yeye yupo juu zaidi ya Amini.
“Unajua soko letu lilivyo linabadilika badilika na hii ni biashara kusema nifuate ‘Ulinah’ sana naweza nikapotea kwa sababu watu walianza kuongea toka kwenye ‘Ole Themba’ lakini ‘Ole Themba’ ni wimbo ambao uliniweka sehemu nzuri sana,” alisema Linah. “Hii hali ya kusema nataka kubaki pale pale inatuangusha sana sisi wasanii ambao tumekuwa pamoja. Yaani tumejiwekea sisi ni wahivi hivi, hapana tunatakiwa tujichanganye ili tubadilike. Kwa sababu mbona yeye bado yupo kule kule lakini yupo wapi?. Usiseme mimi nimepotea yeye mwenyewe yupo wapi? na tukisema kwenye kupotea yeye na mimi nani amepotea?,”
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ amewataka wasanii wenzake kubadilika ili kukabiliana ushindani iliyopo kwenye game.