Bondia kutoka Tanzania Abdallah Pazi Dulla Mbabe alimrambisha sakafu mwenzake kutoka China Zheng Chengbo katika pigano kali lililofanyika usiku wa Ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam.
Dulla iliorushwa ngumi nzito na kumwangusha mpinzani wake na kumfanya kushindwa kuendelea na pigano hilo la uzani wa Light Heavy.
Dulla ambaye alianza pigano hilo kwa kasi na kufanikiwa kumwangusha bondia huyo wa China kwa sekunde kadhaa.
Hatahivyo Chengbo aliamka na kuendelea na pigano.
Bondia wa Tanzania alifanikiwa kumweka Chengbo katika kona na kumrushia makonde makali akimwacha akitokwa na damu chungu nzima katika pua.
Ni wakati huohuo ambapo bondia huyo alishindwa kunyanyuka kutoka sakafuni ndipo refa akamaliza pigano hilo na kumpatia ushindi wa Knock-out Dulla.
Bondia huyo sasa ameshinda mapigano 14 ,13 yakiwa katika njia ya Knockout na kushindwa mara tatu.