Wananchi wamtaka Rais wa Korea Kusini ajiuzulu


Maelfu ya wananchi wa Korea Kusini, waliandamana kwenye mji mkuu Seoul, Jumamosi, kumtaka Rais Park Geun-hye ajiuzulu.


Polisi wamekadiria kuwwa karibu waandamanaji 12,000 walishiriki.

Rais wa Korea Kusini yupo kikaangoni kwa kudaiwa kuvujisha nyaraka za serikali kwa rafiki yake. Wananchi wanataka na mawaziri kadhaa nao wajiuzulu.

Jumanne iliyopita, Bi. Park alikiri kumuonesha rafiki yake Choi Soon-sil nyaraka hizo. Choi ambaye hana nafasi yoyote serikalini, alikuwa akimsaidia Park maoni kwenye hotuba zake kabla ya uchaguzi wa Rais mwaka 2012.

Rais huyo ameomba radhi.