Chris Brown arudisha penzi kwa Rihanna, aanza kutuma zawadi kwa familia ya Riri


Filamu ya mahusiano ya Chris Brown na mwanadada Rihanna yawezekana ikawa inakaribia kuanza tena baada ya Chris kuanza kuonyesha dalili za kurudisha penzi lake kwa Rihanna ambaye kwa sasa anatoka kimapenzi na Drake.

Mtandao wa Hollywoodlife umeripoti kuwa Chris Brown ameanza kutafuta njia ya kuwa karibu na Rihanna kwa kutumia familia ya mwanadada huyo ambapo inasemeka Chris ameitumia zawadi mbambali ili kuonyesha kuwa yupo nayo karibu na ana upendo na familia hiyo.

“Chris Brown amerudi tena kwa Rihanna, amemtuma msaidizi wake Barbados akiwa na vifurushi vyake [Rihanna] na familia yake. Ametuma pombe kali, maua na rundo la midoli kwa ajili ya watoto wote,

“Pia aliweka michoro ambayo ilikuwa imefunikwa na inaonekana alitengeneza mwenyewe. Anasea anataka kumrudisha kwake, ili wawe pamoja. Anaona jambo hilo dhahiri kuwa litavunja mahusiano na Drake na kuwa nafasi yake,” aliandika ripota wa Hollywoodlife.