Aliyekua mwenyekiti wa kitongoji cha Mapinduzi kijiji cha Manga kata ya Mkata Wilayani Handeni Bw Abdalah Bakari umri miaka 40 ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kuchomwa moto na kuutelekeza pembeni kidogo mwa barabara itokayo Mkata Chalinze huku chanzo cha mauaji hayo hakijulikani.
Akielezea tukio hilo kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Shida Bakari amesema kuwa ndugu yao amepotea takribani siku mbili na ndipo wakaanza harakati za kumtafuta ndipo wakakuta akiwa tayari ameshauawa.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha manga wameelezwa kusikitishwa na tukio hilo.
Hata hivyo kutokana na marehemu huyo mwili wake kukutwa eneo la kijij jirani cha Manga ambacho ni mkoa wa Pwani na yeye mwenyewe alikuwa mkazi wa manga ambapo ni Mkoa wa Tanga suala hilo lilichelewesha mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi lakini kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Bonaventura Mushongi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.