Kampuni ya China kuboresha miundo mbinu Dodoma

Mwenyekiti wa kampuni ya ujenzi (CRCC) China, Fengchao Meng, ameahidi kuwekeza kwa kuisaidia serikali katika kuboresha miundo mbinu ya mkoa wa Dodoma.
Ameyasema hayo Jumatatu hii jijini Dar es Salaam, alipokutana na waziri mkuu, Kassim Majaliwa na kusema kampuni hiyo itaungana na serikali katika kuboresha miundo mbinu ya Dodoma.
“Kampuni yangu itaungana na serikali katika kuboresha makao makuu ya serikali, tunatarajia kutuma wataalamu wetu mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya wawekezaji”, amesema Meng.