Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, anatarajia kufanya mahojiano ya moja kwa moja na wasichana 25 wa kitanzania lengo likiwa ni kumwezesha msichana katika masuala mbalimbali ya upatikanaji wa fursa.
Majadiliano hayo yatafanywa na Shirika la Plan International Tanzania na yatafanyikia katika ubalozi wa Marekani, wakati wa maadhimisho ya siku ya msichana duniani, Jumanne hii Oktoba 11, 2016.
Mkurugenzi mkazi wa Plan International, Jorgen Haldoresn, alisema katika kuadhimisha siku hiyo wadau wataombwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kundi hilo na kupewa nafasi ya kujifunza, kuongoza, kuamua na kuishi ili kuonesha thamani ya mtoto wa kike na hata kwa kuwapa fursa sawa.
Mkurugenzi huyo amesema nchi nyingine zitakazoshiriki katika majadiliano na mke wa Obama ni Peru na Cambodia.