Picha: LORI LA BIA LAGONGA KIBERENGE CHA TRENI RELINI SHINYANGA,WATU SITA WAJERUHIWA

Askari polisi wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio,kulia ni kiberenge kilichogongwa na lori lililokuwa limebeba bia leo mjini Shinyanga

Kiberenge cha Treni kikiwa relini baada ya ajali

Lori likiwa limepinduka baada ya kugonga kiberenge cha treni

Bia zikiwa kwenye lori  lililopinduka baada ya kugonga Kiberenge

Lori likiwa limepinduka
Bia zikiwa eneo la tukio
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

TAREHE 08/10/2016.

Taarifa ya tukio la ajali ya gari kugonga kiberenge cha train kwenye njia yake na kusababisha majeruhi pia tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Mnamo tarehe 08/10/2016 majira ya 08:40hrs katika eneo la SGR Barabara ya Shinyanga kuelekea Nzega Kata na Tarafa Mjini, Manispaa na Mkoa wa Shinyanga, gari lenye namba za usajiri T.483AVZ na Trailer T.339AEX aina ya Mecedas Benz mali ya kampuni ya Tanzania Breweries Limited likiendeshwa na Agustini S/O Faustine, 45yrs, msukuma, dereva, mkazi wa Nyakato Mwanza akiwa anatokea Tabora kwenda Mwanza aligonga Kiberenge cha Train namba PGT 5 aina ya Geismar na kusababisha majeruhi kwa wafanyakazi wa TRL waliokuwa ndani ya Kibelenge hicho.
 
 Watu watano na dereva akiwa wa sita wamepata majeraha, ambao ni: 1. Omary S/O Said, 50yrs, myao, mkazi wa Shinyanga ameumia kichwani na mguu wa kulia, 2. Abdallah S/O Maganga, 45yrs, mnyamwezi na mkazi wa Ndembezi ameumia kifuani, 3. Petro S/O Ngasa, 37yrs, msukuma, mkazi wa Shinyanga vidole vitatu vya mguu wa kulia vimekatika, 4. Watae S/O Hussein, 48yrs, mkazi wa Shinyanga ameumia kichwani na kidole cha mkono wa kulia. 5. Joseph S/O Kazungu, 44yrs, msukuma, mfanyakazi wa TRL na mkazi ni Shinyanga ameumia mguu wa kushoto na mgongo.
 
 Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa makini wakati wa kuvuka reli. Majeruhi wamefikishwa Hospital ya Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu.

(2) Mnamo tarehe 08/10/2016 majira ya 00:30hrs katika Kijiji na Kata ya Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo, Wilaya ya Shinyanga na Mkoa wa Shinyanga kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo haijasajiriwa (Guest bubu) mtu mmoja akiwa na bunduki na wenzake sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki ambayo hajafahamika aina yake na mapanga walivunja nyumba hiyo na kumjeruhi Emmanuel S/O Machibya, 31yrs, msukuma, dereva na mkazi wa Solwa kwa kumpiga risasi tumboni pia Neema D/O John alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali mkono wa kulia pia Justin S/O Triphon alishambuliwa kifuani na Charles S/O Marwa alijeruhiwa maeneo ya mikononi na miguuni na panga kisha kupora Tshs 3,160,000/= kwa wahusika hao. 
 
 waliokuwa wamelala katika nyumba hiyo na Gram 3.9 za dhahabu yenye thamani ya Tshs.292,500/= mali ya Samaka D/O Spembo. 
 
Chanzo cha tukio ni kuwania mali. 
 
Aidha majeruhi Emmanuel S/O Machibya amelazwa katika ya Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na majeruhi wengine wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.
 
 Watuhumiwa July S/O Lutwe, 41yrs, muha, mlinzi, mkristo, mkazi wa Kahama na wenzake wanne wanashikiriwa kwa mahojiano.

Muliro J. MULIRO - ACP

KAMANDA WA POLISI MKOA