VIDEO: Mapendekezo ya Zitto Kabwe kuhusu kuboresha suala la Elimu nchini

Leo October 8 2016 chama cha ACT Wazalendo kimefanya mkutano mkuu wa kidemokrasia katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa Posta Jijini Dar es salaam. Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewasilisha hotuba yake ya ufunguzi na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu hali ya nchi kwa mtazamo wa chama.
Katika hotuba yake hiyo Zitto Kabwe ameizungumzia udhaifu wa suala la Elimu nchini ambapo amesema…..>>>Ujinga una gharama kubwa mno katika nchi, vitendo vingi vya ovyo tunavyovishuhudia katika siku za karibuni kama vile kuchoma watu moto ni tunda la ujinga unaotokana na elimu duni.
Hata hivyo katika hotuba yake zitto amependekeza haya……>>>kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi unaonesha kuwa walimu ndio msingi mkuu wa kujifunza na kuboresha elimu chama chetu kinahimiza kuwekeza katika kuweka mfumo imara wa motisha na uwajibikaji kwa walimu, tunasisitiza katika kuwekeza katika mafunzo ya walimu na kuhakisha walimu wanawlipwa katika  kiwangoo ambacho kitawawezesha kukabiliana na maisha uko walipo
>>>Tafiti zinaonyesha mtoto hujifunza vizuri zaidi kama atatumia lugha anayotumia nyumbani wakati wa kujifunza darasani, ukweli ni kwamba kutokana na mazingira duni ya kujifunza lugha ya kiingereza watanzania wengi hawamudu lugha hii na imekuwa kikwazo katika kujifunza, katika kutatua changamoto ya lugha ya kujifunza nchini msimamo wetu ni kuwa na mfumo pacha wa lugha ya kufundisia yaani billngual education system, katika mfumo huu kiswahili na kiingereza vitatumika sambamba kama lugha za kutoa na kutafuta maarifa.:-Zitto kabwe