Fursa za kibiashara ambazo zimekuwa zikiizunguka klabu ya Real Madrid zimewashawishi viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na Rais Florentino Perez kuja na mkakati mpya wa kufanya maboresho ambayo yataufanya uwanja wa klabu, Santiago Bernabeu kuwa katika mwonekano.
Marekebisho ya uwanja huo yatakamilika mwaka 2020 na yatagharimu Pauni Milioni 360 hadi kukamilika, marekebisho ambayo yataufanya uwanja huo kuwa katika mwonekano tofauti ambao una lengo la kibiashara.
Aidha pamoja na marekebisho hayo, uwanja utaendelea kuwa na uwezo wa kuingiza watu 80,000 na ofisi za klabu zilizokuwepo katika uwanja huo zikihamishwa ili kupisha upanuzi wa sehemu ya makumbusho ya klabu.
Pia Real Madrid itabadili jina la uwanja huo na kuwa na jina la kampuni ambayo itagharamia marekebisho ya uwanja huo na kuwa katika mwonekano ambao wanahitaji.
Mwonekano wa Real Madrid, Santiago Bernabeu baada ya kukamilika marekebisho mwaka 2020.
Meya wa jiji la Madrid, Manuela Carmena akionyesha jinsi uwanja wa Santiago Bernabeu utakavyokuwa baada ya marekebisho, kushoto ni Rais wa Real Madrid, Florentino Perez.
Mwonekano wa sasa wa uwanja wa Santiago Bernabeu.