Rais Mstaafu Kikwete ashindwa Kuvumilia, Atoa Onyo kuhusu Picha Zake Mitandaoni

Rais mstaafu kutoka kwenye awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni.
Kupitia Twitter page yake Mstaafu JK ameandika >>> ‘Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa
Nimestaafu naomba niachwe nipumzike nisingependa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya serikali… namuunga mkono Rais na Serikali yake‘ – Jakaya Kikwete.
screen-shot-2016-10-27-at-11-20-45-pm