Uongozi wa Young Africans Sports Club umekanusha habari ambazo zimekuwa zikisambazwa zikisema Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club amejiuzulu wadhifa huo.
Katika taarifa uliyoitoa uongozi wa Yanga umesema unasikitishwa na habari hizo na unawaomba wanachama wote kuupuzia ujumbe huo wenye malengo ya upotoshaji, pia unazidi kuwakumbusha wanachama kuwa habari sahihi zinatolewa na uongozi huo na si vinginevyo!
Bw Yusuf Mehbob Manji bado ni Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club!
Imetolewa na
Uongozi wa Young Africans Sports Club
Daima Mbele Nyuma Mwiko!