Jay Z Haji Ng'o Kwenye Fiesta 2016, Ufafanuzi Watolewa

Tamasha la burudani la Fiesta 2016 limekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba watamleta msanii wa Marekani Jay Z katika show ya Fiesta Dar es salaam.


Mapema Jumamosi hii zilisambaa picha ‘fake’ inayomuonyesha msanii huyo mahiri duniani akiwa ameshasajiriwa kwa ajili ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 5 katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Clouds FM umetoa taarifa hii:
Kumetokea uzushi kwamba tumemsajili msanii Jay Z kwa ajili ya kilele cha #Fiesta2016 hapo #November05. Tunapenda kukanusha habari hiyo; picha iliyotengenezwa kueneza habari hiyo ni batili
Wasanii wakimataifa ambao tayari uwepo wao umetangazwa ni pamoja na Yemi Alade wa Nigeria, Jose Chameleone wa Uganda pamoja na Tekno wa Nigeria.
Hii ni list ya wasanii wa Tanzania.
1. Ben Pol
2. Nandy
3. Christian Bella
4. Fid-Q
5. Weusi
6. Roma
7. Chegge
8. Dogo Janja
9. Billnass                              
10. Stamina
11. Jux
12. Barnaba
13. Maua Sama
14. Darassa
15. Vanessa Mdee
16. Sholo Mwamba
17. Jay Moe
18. Msami
19. Juma Nature
20. Snura
21. Baraka Da Prince
22. Shilole
23. Manfongo
24. Belle 9
25. Lord Eyes
26. Young Dee
27. Raymond
28. Mr. Blue
29. Alikiba – Kingkiba
30. Hamadai