Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela leo ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person of the Year #POY2016).
Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile uchumi, siasa, utamaduni.
Thuli Madonsela
Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Mwaka 2015 tuzo hii ilikwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MeTL, Mohammed Dewji.