JANUARI 2017, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake, Barack Obama ataondoka kwenye Ikulu ya nchi hiyo, White House na kuelekea kwenye makazi yake mapya huku akimuachia Donald Trump atakayekuwa ameshika dola.
Huu hapa mjengo aliyoukodi Obama kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake mara baada ya kuondoka White House.
Mjengo huo ambao unamilikiwa na Joe Lockhart umejengwa mwaka 1928, una eneo la futi za mraba 8200 karibu na Washington DC ambao Obama ameukodi kwa gaharama ya dola milioni 5.3 sawa na bilioni 11,5 za Kitanzania.
Obama ataishi humo na familia yake mpaka pale ambapo mwanaye wa pili, Sasha atakapomaliza masomo ya High School.