VIDEO: Waziri Mwakyembe alishindwa kujizuia na kumwaga machozi akimuombea Samwel Sitta





November 11 2016 wabunge pamoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa waliungana kwa pamoja kutoa salamu zao za mwisho kwa spika mstaafu Samuel Sitta aliyefariki dunia akiwa nchini Ujerumani akipatiwa matibabu.

Kila mmoja aliguswa kwa namna yake katika msiba huo akiwemo Waziri wa katiba na sheria Dr. Harrison Mwakyembe ambaye hakuweza kujizuia kuangusha machozi pale alipopewa nafasi ya kumuombea marehemu..