Fid Q: Wakazi na Nikki Mbishi si wanahiphop wa kuchukuliwa poa


Rapper Fid Q amewataja wasanii wawili wanaofanya muziki wa Hip Hop ambao wanachukuliwa kikawaida lakini wakipewa nafasi zaidi mwakani wanaweza kufanya vizuri.

Fid Q amewataja Wakazi pamoja na Nikki Mbishi ni wasanii ambao anawakubali kutokana na juhudi zao na kujituma kwenye muziki lakini pia wanatakiwa kupewa nafasi zaidi mwaka ujao.

“Kukweli mimi napenda sana juhudi za Wakazi amekuwa akijituma sana lakini pia kuna msanii anaitwa Nikki Mbishi amekuwa akitoa ngoma nyingi sana kali lakini watu ni kama wameamua kulala tu juu yake. Nafikiri 2017 mnapaswa kuwazingatia watu kama kina Niki Mbishi sababu wanafanya vizuri,” Fid Q amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

“Unajua unapokuwa msanii mzuri na unaona watu kama hawana mpango na wewe kidogo inaweza kuku-frustrate na ikaleta shida mbeleni. Kwahiyo tujaribu kuangalia kuona jinsi gani tunaweza kubeba vipaji vya wasanii wetu wengine ili tuweze kuinua hii platform na kuutangaza utaifa vyema,” ameongeza.