PICHA: MASELE CHAPOMBE AFUNGA NDOA




Msanii wa vichekesho aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia Kundi la Vituko Shoo, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’ ameaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Specioza Malick iliyofungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam.