Mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu Mkoani Geita, Elisha Sylvester (26) amelazwa katika wodi nane katika Hospitali teule ya Mkoa wa Geita huku akiwa hajitambui baada ya kudaiwa kupigwa na raia wawili wa China
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani hapa baada ya Julai 6 mwaka jana mkazi wa Kijiji cha Nyamitondo tarafa Butundwe
, Masanja Shilomero (25) kushambuliwa na mwajiri wake ambaye ni raia wa China Myo baada ya kuomba kupandishiwa mshahara
Hata hivyo Sylvester anadaiwa kufanyiwa unyama huo Januari 19 mwaka huu ndani ya mgodi unaomilikiwa na wachina hao uliopo katika kijiji cha Mawemeru, Kata ya Nyarugusu wilayani Geita
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa wachina hao ambao majina yao hayakupatikana walimshambulia kijana huyo ambaye ni Mfanyakazi wa mgodi huo kwa fimbo, ngumi na mateke baada ya kumtuhumu kuiba mawe mawili ya dhahabu
"Baada ya kijana huyo kupigwa, alifikishwa katika kituo kidogo cha polisi Nyarugusu na kuchukuliwa maelezo kisha kupewa PF3 na kulazwa kwenye zahanati ya Nyarugusu akipatiwa matibabu". alidai shuhuda huyo.