Mugabe atatimiza miaka 93
Chama kinachotawala nchini Zimbawe Zanu-PF, kimeanza kuchangisha pesa kwa sherehe za siku ya kuzaliwa ya Rais Robert Mugabe ambaye anahitimiza miaka 93.
Waandalizi wa sherehe hizo wanasema kuwa wanataka kuchangisha ng'ombe 150 kwa chakula.
Gazeti la serikali la Herald limemnukuu mbunge Never Khanye, akisema kuwa hakuna mtu atalazimishwa kuchanga lakini wakulima wakubwa katika maeneo ya matabeleland ambapo shehere zitafanyika, ni lazima watoe ngombe mmoja kila mmoja, kutoa asante kiongozi huyo wa miaka mingi.
Wakulima wakubwa ni wale walipata mashamba makubwa kutoka kwa serikali kufuata hatua ya serikali ya kunyakua mashamba kutoka wa wazungu wakati wa programu iliyokumbwa na utata nchini Zimbabwe.
Chama cha Zanu-PF kinasema kuwa kinatarajia karibu watu 100,000 kuhudhuria sherehe hizo.
Shere hizo zitafanyika eneo la Matobos nje kidogo ya mji wa Bulawayo.