HAYA NDIYO MAMBO 5 YANAYOUMIZA WENGI KATIKA MAHUSIANO





1. Kuna jambo huwezi ficha: Kuna jambo hata ukijaribu kulificha, ukweli wake utajulikana tuu hususani kama utakuwa na mahusiano ya muda mrefu na mtu husika. Jambo hilo ni ukweli  kama unampenda kwa dhati mwenza wako au la. Mpenzi wako akiwa makini atagundua ‘kufeki’ kwako , kutokana na matendo yako hususani vile unavyojali hisia zake, usikivu wako kwake, heshima yako kwake, na unavyojali umoja na kudumu kwa uhusiano wenu.

2. Fedha sikuzote itawasumbua: Hata kama mtajitahidi kupuuzia umuhimu wa fedha katika mahusiano yenu, fedha itabaki kuwa mhimili mkubwa wa mahusiano yenu. Hata kama nyote mna ingiza kipato kuna changamoto mtazipata kama vile kupanga kwa pamoja jinsi ya kutumia fedha zenu, au kujieleza kuhusu matumizi fulani ambayo mwenzi wako atahoji. 
3. Kazi ya ziada: Haijalishi una hisia na makusudio mazuri sana, bila matendo yanayomridhisha mpenzi wako, hautoweza kujenga furaha ya kweli katika mahusiano yenu. Ni muhimu pia kutambua kwamba pamoja na kuwa na makusudio na matendo mazuri, inakupasa kutilia mkazo kuwa matendo yako na makusudio yako yanaaminika kwa mpenzi wako.

4.Kuna mambo hautokaa ujue ukweli wake: Haipendezi ila ndio uhalisia kuwa pamoja na ukweli kwamba nyie mmeshibana katika mahusiano yenu, bado kutakuwepo na siri ambazo haitaambiana. Mbaya zaidi katika siri hizo, inaweza kuwepo siri ya hisia halisi kuhusu upendo wa mpenzi wako kwako, au upendo wako kwake. Mfano, wapo waliooana lakini mmoja wapo sio kwamba kweli anampenda mwenzake, ila alitaraji kujenga upendo akiwa kwenye ndoa, na kweli anapokuwa kwenye ndoa anajikuta amejenga kumjali mpenzi wake, hatimaye anajikuta ameweza kumpenda moja kwa moja. 

5.Makosa haya ni magumu sana kusahaulika: Kwa kawaida binadamu wengi hukumbuka mabaya kwa urahisi kuliko mazuri tunayowafanyia. Na katika mahusiano, makosa haya mawili ; kwanza ni ‘ku cheat’ na pili kutokuonyesha mvuto wa kimapenzi kwa mpenzi wako, yanaweza kuwa makosa ambayo si rahisi kusahaulika, ingawaje mtu atajitahidi kusamehe, na kujaribu kufanya mahusiano yaende kawaida.