Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo Jumapili October 30 2016.
Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika
basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo tutawaletea taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.
Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto
Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.
Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na lori hilo.

Angalia video hapa chini Basi la Safari Njema likiteketea kwa moto