Breaking News: Huyu Ndiye Mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016

Mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 Olive
Mkenya, Olive Kiarie pichani juu, ameibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha Sh30 milion katika shindano la Maisha Plus East Africa 2016 lililoandaliwa na Kampuni ya DMB.

Shindano hilo lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na walikaa kijijini kwa wiki nane tangu Septemba 4.

Washiriki 16 pekee ndiyo walioingia fainali usiku huu katika fainali za shindano hilo zilizorushwa na Kituo cha Televisheni cha Azam.

Awali, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alizindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka iliyoundwa na washiriki wa shindano hilo katika kijiji cha Maisha Plus East Africa 2016.