Kwa miaka mingi mfululizo, haijawa rahisi kwa shindano la Miss Tanzania kumalizika bila malalamiko, lawama au kashfa. Awamu hii pia, yamekuwepo malalamiko kadhaa kuhusiana na maandalizi yake na jinsi shindano lilivyofanyika huku kukiwepo kasoro kadhaa.
Lakini mrembo aliyewahi kushiriki shindano hilo miaka ya nyuma, Jokate Mwegelo, ameyatetea mashindano hayo akisema kuwa waandaji wamefanya kazi nzuri na wanastahili pongezi. Haya ni maelezo yake aliyoandika kupitia Twitter.
Fainali za mashindano ya Miss Tanzania zitafanyika Mwanza kwa miaka mitatu zaidi. Brilliant idea. I support this move. Open up mikoa zaidi. Ukiacha mapungufu fainali za Miss Tz ni shindano pekee la urembo ambalo huwezi kusikia mshindi amedhulumiwa zawadi yake au show ikapwaya.
Show ya Mwanza ilifanyika nje viingilio 100k,50k,20k na ilijaa watu licha ya mapungufu ya production. Nilikuwepo so najua ninachoongea.
Wadada wawili walipewa jukumu la kusimamia fainali hizi. Hao wadada wanakaa mkoani Mwanza. Nawapongeza kwa kufanikisha licha ya changamoto.
Kamati just needs to perfect the craft of moulding contestants to be competitive and of coarse giving us the ideal winner who will thrive. Ni rahisi sana kuchambua na kukosoa mashindano haya humu ila ukilinganisha na mashindano mengine ya urembo nchini angalau wanafanya vizuri.
Wanafanya vizuri kufikia warembo wengi kupitia mikoa mbalimbali na sio DSM tu au mikoa ya karibu. Vipaji vinatoka sehemu mbalimbali.
We need a sole company to deal na production. Creative themes and execution. Sio tu kwenye show za urembo na kwenye matamasha mengine.