Ufafanuzi kuhusu umri wa Miss Tanzania 2016 Diana Edward Loy watolewa

Usiku wa Jumamosi, mrembo wa Kinondoni, Diana Edward Loy alitwaa taji la Miss Tanzania 2016 katika fainali zilizofanyika jijini Mwanza.

Miss Tanzania 2016, Diana akiwa na warembo wengine wa top 5 baada ya kutangazwa mshindi
Hata hivyo pamoja na ushindi huo, haikuchukua muda akaanza kuubeba mzigo wa umaarufu kwa kusambaa taarifa zinazohusiana na umri wake.
Taarifa iliyosambaa ilisema:
MISS TANZANIA 2016
🙊🙊🙊🙊🙊🙊
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
😂😂😂😂😂😂
Ingawa sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili.

Kaimu afisa habari wa mrembo huyo, Charles William amelazimika kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya habari za mshindi huyo:
Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;
1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.
2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.
3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.
4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya “Character assassination” lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.
Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atul
etee Taji la Dunia.