Kim Kardashian aishitaki tovuti ya udaku iliyodai amedanganya kuvamiwa Paris

Kim Kardashian anadai kuwa ameathirika tena, awamu hii na tovuti ya udaku iliyoripoti kuwa alidanganya kuvamiwa na watu wenye silaha na kuporwa, kisha kutaka alipwe bima ya mamilioni ya dola kwa mali alizopoteza.
Kwenye kesi hiyo iliyofunguliwa Manhattan Jumanne hii, Kardashian, 35, anasema MediaTakeOut.com iliandika habari ya kumchafua yenye kichwa cha kupotosha kuwa alikuwa muongo na mwizi kwa kutengeneza tukio hilo.
Maelezo yenye kurasa nane ya shitaka hilo, yanadai kuwa licha ya maisha yake kuwa hatarini, Kim amekuja kuumizwa zaidi na taarifa hiyo kuwa alipanga kila kitu.
“Kardashian was assaulted and robbed by two masked men, who placed a gun to her head, duct-taped her hands, legs and mouth, and then left her lying helplessly on the bathroom floor of her rented apartment while the thieves absconded with millions of dollars in jewelry,” yamesema maelezo.
Habari ya tovuti hiyo imesema Kim alitengeneza kisa hicho ili kutengeneza kiki ya show yake ya TV. Media Take Out inadaiwa kukataa kuifuta habari hiyo na imegoma kumuomba radhi.
Kim anataka mmiliki wa tovuti hiyo Fred Mwangaguhunga kumlipa kiasi kisichojulikana cha fedha kwa madhara aliyoyapata.