Mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii, Ephrahim Kwesigabo, amesema mfumuko wa bei wa taifa wa Septemba mwaka huu umepungua mpaka kufikia asilimia 4.5 kutoka 4.9 ilivyokuwa Agosti.
Mkurugenzi huyo amesema bidhaa za chakula zilizopungua bei ni samaki, dagaa,na viazi vitamu.
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 97.04 kwa Septemba mwaka huu kutoka Disemba 2015,ikilinganishwa na shilingi 96.83 iliyokuwa Agosti 2016”, alisema Kwesigabo.
Aidha alisema kwa upande wa bidhaa zisizo za chakula zilizopungua ni pamoja na gesi,petroli na dizeli.