Nadal, Federer kwa mara ya kwanza watupwa nje nne bora ikiwa ni katika muda wa miaka 13

Wachezaji nyota wawili wa mchezo wa tenesi Rafael Nadal na Roger Federer kwa mara ya kwanza wamekosekana kwenye nafasi nne za juu za ubora wa viwango vya mchezo wa tenesi dunia hii ikiwa ni katika muda wa miaka 13.

Rafael Nadal na Roger Federer
Kwa wakati tofauti nyota hawa walishawahi kushika nafasi ya kwanza ya viwango vya ubora wa mchezo huu.
Rafael Nadal ambaye kwasasa ana umri wa miaka 30 anashika nafasi ya tano huku Roger Federer akiwa katika nafasi ya saba kwa ubora.
novak-djokovic-miami-open-tennis_3284770
Novak Djokovic
Mserbia Novak Djokovic ndie ameshika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya mchezo huo duniani.
Orodha kamili ya wachezaji bora
1 Novak Djokovic
2 Andy Murray
3 Stan Wawrinka
4 Kei Nishikori
5 Rafael Nadal
6 Milos Raonic
7 Roger Federer
8 Gael Monfils
9 Tomas Berdych
10 Dominic Thiem