Ajuta kuuvisha Uume wake Pete..Makubwa yamkuta, Madaktari washindwa Kuitoa

Iliripotiwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 28 mjini Johannesburg alijivisha pete hiyo “kwa sababu za kujiburudisha kimahaba” lakini aibu kwake, kwani ilibidi akimbizwe hospitalini na mamake mzazi.
Kulingana na mashirika ya habari, alifikishwa hospitalini akiwa na maumivu makali na jongoo lilikuwa limegeuka kuwa rangi ya samawati.
Baadaye alisemekana kukiri alijivisha pete “kufuatia pendekezo la marafiki wake”.
Madaktari walishindwa hata kuikata pete hiyo na ikawalazimu kumpa dawa za kulala kisha wakamfanyia upasuaji kutoa damu iliyokuwa imesababisha kuvimba kwa jembe la jamaa huyo.
Upasuaji wenyewe ulifanywa kwa kutumia sindano ambayo alidungwa nayo mara kadha huku damu ikitolewa hadi uvimbe ukapungua kisha pete ikatolewa.