Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11, mkazi wa Buguruni Madenge jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam amedaiwa kufanyiwa vitendo vya ulawiti na kijana aliyejulikana kwa jina la Kulwa Omera anayetajwa kuwa ni dereva wa bodaboada katika kituo cha Buguruni Sheli jijini humo ambae anadaiwa kutoweka na kwenda mahali kusikojulikana mara baada ya tukio hilo kufanyika.
Akizungumzia tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo Lucia Stephano amesema kuwa aligundua mtoto wake kafanyiwa unajisi mara baada ya kuona mtoto huyo akitokwa na haja kubwa isivyo kawaida kitendo ambacho kilimlazimu mama huyo kumhoji mtoto ambapo kwa mujibu wa mtoto alidai kufanyiwa vitendo hivyo kwa zaidi ya mara tatu na kijana Kulwa Omera.
Baada ya kupata maelezo kutoka kwa mama wa mtoto pamoja na mtoto aliyefanyiwa vitendo hivyo mwandishi wa habari hii alifika eneo ambalo kilikuwa ni kituo cha kazi cha Mtuhumiwa Kulwa Omera cha Buguruni Sheli na kuzungumza na baadhi ya madereva wa boda boda wanaodaiwa kufanya nao kazi
Kwa mujibu wa Dawati la Jinsia na watoto la Kituo cha Polisi cha Buguruni wanaendelea na juhudi za kumkamata kijana Kulwa Omera ili kujibu tuhuma hizo.
Chanzo:Channel ten habari