Imesemekana watu wengine 22 walilazwa hospitalini katika mji wa Abong-Bang ulio mashariki mwa nchi baada ya kunywa pombe hiyo inayofahamika kama odontol.
Kituo cha habari cha CRTV kilisema maafisa wa serikali walipiga marufuku utengezaji na uuzaji wa pombe hiyo baada ya vifo hivyo kutokea.
Odontol hutengezwa kwa kutumia mnazi, sukari na maganda ya miti kisha kuuzwa katika maduka ya kienyeji kwa bei ya chini. Wakati mwingine vitu vingine huongezwa kwenye pombe hiyo kuifanya iwe kali zaidi na huweza kugeuka kuwa sumu.
Kulingana na CRTV, watu 18 walifariki Mindourou na wengine watatu wakafa Abong-Bang, na baadhi yao ni wanawake.
Mmoja wa wanawake aliyetambuliwa kama Angeline ambaye ni miongoni mwa waliolazwa hospitalini alisema alikunywa tu glasi mbili za odontol.
Imekusanywa na VALENTINE OBARA